Hafla ya maombolezo ya siku ya saba ya mwezi wa Muharram imefanyika katika Shule ya Imam Zainul Abidin (a.s) mjini Bujumbura, Burundi, ikijumuisha usomaji wa Qur’an, Ziara ya Ashura na hotuba kuhusu dhana ya uaminifu katika Uislamu.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Majlisi ya maombolezo ya siku ya saba ya Muharram imefanyika tarehe 24/06/2026 katika Imam Zainul Abidin School mjini Bujumbura nchini Burundi.
Hafla hiyo imeanza kwa usomaji wa Qur’an ulioongozwa na mwanafunzi Abdulkarim Ayyoub, kisha kufuatiwa na usomaji wa Ziara ya Ashura uliofanywa na Sheikh Khamis Sadiq.
Baadaye, Sheikh Saeed alitoa hotuba maalumu yenye mada isemayo “Uislamu ni Amana,” ambapo alisisitiza umuhimu wa kuilinda dini, maadili na majukumu ya Kiislamu kama amana kubwa aliyopewa mwanadamu.
Majlisi hiyo iliendelea kwa maombolezo na tenzi zilizoimbwa na mwanafunzi Jafar Mohsin, zikikumbusha tukio la Karbala na shahada ya Imam Hussein (a.s.) pamoja na wafuasi wake.
Waandaaji wa hafla hiyo wamesema kuwa maadhimisho hayo yanalenga kuhuisha ujumbe wa Ashura na kuimarisha maadili ya uadilifu, uaminifu na kujitolea ndani ya jamii ya Kiislamu nchini Burundi.
Your Comment